MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA (FAQs)

1. Je, Winprints mnaprint bidhaa gani?

Tunaprint T-shirt, vikombe, chupa, kofia, vitambaa, na bidhaa zingine kwa ajili ya matangazo au matumizi binafsi. Pia tunatengeneza picha mbao na picha saa za ukutani.

2. Mnafanya branding ya aina gani?

Tunafanya branding ya bidhaa (product branding), branding ya kampuni (corporate branding), pamoja na branding kwenye vifaa kama magari, mabango, mabox, na mavazi ya kampuni.

3. Naweza kuagiza T-shirt zenye muundo wangu mwenyewe?

Ndiyo kabisa. Tunakubali design kutoka kwa mteja au tunaweza kukusaidia kuibuni kwa ajili yako bila gharama ya ziada ya ushauri wa awali.

4. Mnatumia aina gani ya printing kwenye T-shirt?

Tunatumia teknolojia mbalimbali kama Screen printing, DTF (Direct to Film), Sublimation nk kulingana na aina ya kazi na mahitaji ya mteja

5. Je, kuna kiwango cha chini cha oda (minimum order)?

Kiwango cha chini kinategemea aina ya bidhaa. Kwa mfano:

T-shirt: kuanzia moja (1)

Vikombe: kuanzia kimoja (1)

Mifuko ya kuchapa: angalau kumi (10) Kwa oda kubwa tunatoa punguzo maalum.

6. Muda wa kutayarisha kazi ni kiasi gani?

Kwa kawaida ni siku 1 hadi 3 kwa kazi ndogo, na siku 3 hadi 7 kwa oda kubwa au kazi maalum. Tunalenga kumaliza kwa wakati bila kuchelewa.

7. Je, mnafanya delivery ya bidhaa?

Ndiyo. Tunatoa huduma ya delivery ndani ya mkoa na hata nje ya mkoa kupitia usafirishaji (bus, cargo).

8. Ninawezaje kuwasiliana nanyi kwa haraka?

Unaweza kututumia ujumbe kupitia WhatsApp kwa namba: 0757003774 au kutupigia moja kwa moja. Pia tupo Instagram @winprints_ na Facebook kwa jina @winprints.

9. Je, mnatengeneza logo na graphics nyingine?

Ndiyo. Tunatengeneza logo, banner, brochures, business cards, na kazi nyingine za kisasa za graphic design.

10. Mnatoa ushauri wa aina ya design au branding bora kwa biashara yangu?

Ndiyo. Tunatoa ushauri wa kitaalamu kuhusu design na branding kulingana na aina ya biashara yako au hadhira unayolenga.

11. Je, picha saa na picha mbao ni za ukubwa gani?

Tunatengeneza kwa ukubwa mbalimbali kama A4, A3, A2 hadi A1. Unaweza pia kuagiza ukubwa maalum kulingana na hitaji lako.

12. Mnachapisha ID cards pia?

Ndiyo, tunachapisha ID cards za wafanyakazi, wanafunzi, matukio, mashindano n.k., kwa ubora wa hali ya juu.

13. Mnaweza ku-print jina la mtu mmoja mmoja kwenye bidhaa?

Ndiyo. Tunaweza kuchapisha majina binafsi kwenye T-shirt, vikombe, penseli, notebooks, kofia n.k. Hii ni bora kwa zawadi na sherehe.

14. Je, gharama zenu zikoje?

Gharama hutegemea aina ya kazi, idadi ya bidhaa na design. Tunatoa bei nafuu kulingana na bajeti ya mteja na kazi husika. Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.

15. Ofisi zenu zipo wapi?

Tunapatikana Arusha mjini karibu na stand kuu na Longido mjini pia tunapokea oda kwa njia ya mtandao kupitia WhatsApp na mitandao ya kijamii.